Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayataka mataifa ya Asia kuchukua uongozi wa masuala ya dunia

Ban ayataka mataifa ya Asia kuchukua uongozi wa masuala ya dunia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa ya Asia na Pacific kuchukua uongozi wa dunia hususani kwenye masuala ya kimataifa yakiwemo ya upatikanaji wa chakula, kawi, haki za binadamu na suala la kuwainua wanawake. Akiongea pembeni mwa mkutano wa ASEAN kwenye kisiwa cha Bali nchini Indoneshia Ban amesema kuwa huu ni wakati wa nchi za Asia kuchukua wajibu wa dunia.

Ban amesema kuwa maendeleo ndiyo ajenda kuu kwenye ushirikiano kati ya UM na mataifa ya ASEAN akiongeza kuwa mataifa hayo yanaelewa masuala kadha yakiwemo ya mabadiliko ya hali ya hewa, uhaba wa maji na nishati, suala la afya duniani pamoja na usalama wa chakula na lishe.