Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka kutengwa fedha zaidi katika udumishaji usafi

Mtaalamu wa UM ataka kutengwa fedha zaidi katika udumishaji usafi

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kuwa na maji safi ya kunywa na usafi Catarina de Albuquerque amezitaka serikali kutenga fedha zaidi zitazotumika katika kuporesha usafi akiongeza kuwa watu wana haki ya kuwa vyoo vya kisasa.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya choo duniani mtaalamu huyo amesema kuwa ukosefu wa usafi umechangia katika kuongezeka kwa gharama za afya. De Albuquerque ameongeza kuwa mataifa yanaweza tu kuongeza miaka ya watu kuishi na kupunguza vifo vya watoto ikiwa tu yatawekeza zaidi katika udumishaji usafi.