Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu kuzuru Bali na Maldives kuanzia Jumanne

Mkuu wa haki za binadamu kuzuru Bali na Maldives kuanzia Jumanne

Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay Jumanne aataanza ziara ya wiki moja barani Asia, akianzia Maldives ambako atajadili masuala ya kikanda na kitaifa kabla ya kuelekea Bali Indonesia ambako atahudhuria mikutano kuhusu haki za binadamu ya kanda ya Asia.

Maldives ambako atakuwa tarehe 22 hadi 24 November atakutana na Rais Mohamed Nasheed, viongozi wengine wa kisiasa, tume ya kitaifa ya haki za binadamu na jumuiya za kijamii. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)