Wazimbabwe takribani milioni 1 wakabiliwa na njaa:WFP

21 Novemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema zaidi ya Wazimbabwe milioni moja wanahitaji msaada wa chakula na limeomba dola milioni 42 kutoka kwa wahisani ili kisaidia Zimbabwe.

Kwa mujibu wa WFP familia nyingi tayari zimepunguza idadi ya milo katika kipindi hiki cha palizi ambacho kinatarajiwa kumalizika mwezi Machi kwa mavuno. Shirika hilo linasema maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale makavu nchini humo na yanatarajiwa kupata mavuno kidogo sana.

Katika taarifa WFP iliyotolewa Jumatatu Harare inasema familia masikini hususani za yatima, na watoto haziwezi kumudu kununua chakula kilichopo kwani chakula kingi kinaingizwa toka nje na gharama ni kubwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter