UM washitushwa na ghasia na ukiukwaji wa uhuru katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge Misri

21 Novemba 2011

Kundi la wataalamu wa uhuru wa Umoja wa Mataifa Jumatatu wameelezea hofu yao kuhusu kiwango cha ghasia na kuzorota kwa uhuru wa kukusanyika kwa amani hali ambayo imesababisha kupotea kwa maisha ya watu nchini Misri.

Ghasia hizo zimezuka wakati taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu. Duru za habari zinasema watu takribani 20 wamepoteza maisha katika ghasia hizo. Monica Morara na taarifa kamili.

(RIPOTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud