Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka Afrika isaidiwe kufikia nishati endelevu

Ban ataka Afrika isaidiwe kufikia nishati endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kushikama ili kuwasaidia watu zaidi milioni 600 barani Afrika ambao wanakabiliwa na hali ngumu ya ukosefu wa nishati.

Ban amesema ni muhimu kutambua kuwa bara la afrika linapaswa kuwekewa msukumo wa pekee hasa katika eneo la uendelezwaji wa nishati mbadala, kwa vile eneo hilo ni muhimu kwenze maeneo ya uchumi na maendeleo

Amesema kuimarishwa kwa vyanzo mbadala vya nishati kutalisaidia bara la Afrika kuondokana na hali ya utegemezi na hivyo kusuma mbele shughuli zake za kimaendeleo.

Katibu Mkuu alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Afrika kuhisiana na mapinduzi ya kiviwanda.