Pillay apongeza kukamatwa kwa Al-Islam na Zennusi ataka watendewe haki

21 Novemba 2011

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatatu amekaribisha hatua ya kukamtwa nchini Libya kwa Saif Al Islam Gaddafi na mkuu wa zamani wa ujasusi wa taifa hilo Abdullah Al Senussi, watu ambao walitolewa kibali cha kumatwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC tangu mwezi Juni mwaka huu.

Pillay amesema kukamatwa kwa mtoto wa Gaddafi na mkuu wa zamani wa upelelezi ni hatua kubwa kwa mustakhabali wa sheria nchini Libya. Amekaribisha pia tangazo la waziri mkuu wa Libya kwamba watu hao watatendewa haki na kushitakiwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Bi Pillay ameutaka uongozi wa Libya kushirikiana ipasavyo na mahakama ya ICC kwa kuzingatia azimio la Baraza la Usalama namba 1970 lenye mtazamo wa kuhakikisha kwamba wote waliohusika na kikaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa wanawajibishwa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter