Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha gesi inayochafua mazingira kinaongezeka:WMO

Kiwango cha gesi inayochafua mazingira kinaongezeka:WMO

 

Kiwango cha gesi gesi chanfu ya viwandani inayoathiri mazingira kimeongezeka na kufikia hali ya hatari mwaka 2010 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO. Ripoti ya shirika hilo inasema kati ya mwaka 1990 na 2010 kumekuwa na ongezeko la asilimia 29 la gesi chafu iliyosababisha ongezeko la joto duniani na hiki ni kiwango cha juu tangu miaka ya kwanza ya uzalishaji mkubwa wa bidhaa za viwandani.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WMO Michael Jarraud shughuli za binadamu zikiwemo kuchoma mafuta asili, kutumia mbolea na kukata miti ni miongoni mwa sababu kubwa na kuongezeka kwa gesi inayoathiri mazingira.

(SAUTI YA MICHAEL JARRAUD)