Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu kufanya kikao maalumu kuhusu Syria

Baraza la haki za binadamu kufanya kikao maalumu kuhusu Syria

 

Ofisi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu limewambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba kikao maalumu kuhusu Syria kinaweza kikafanyika katika wiki chache zijazo. Kikao hicho kitafuatia kuchapishwa kwa ripoti ya tume huru ya uchunguzi dhidi ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu ambayo inakamilishwa mjini Geneva wiki hii.

Uchunguzi huo ulianzishwa na baraza la haki za binadamu baada ya ripoti ya ujumbe uliokwenda kutafuta ukweli wa hali halisi ambao ulielezea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali.

Timu za wachunguzi hivi sasa vimezuiliwa kuingia Syria kwenye majimbo yaliyoghubikwa na machafuko na hivyo kulazimika kufuatilia ukiukwaji huo kutoka kupitia nchi jirani. Kwa mujibu wa Roland Gomez, msemaji wa baraza la haki za binadamu matokeo ya ripoti hiyo yatachapishwa mjini Geneva siku chache zijazo.