Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la kisukari linaongezeka nchini Burundi

Tatizo la kisukari linaongezeka nchini Burundi

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama ya moyo, saratani, matatizo ya kupuma na kisukari yamekuwa yakileta mzigo mkubwa sio tu kwa familia, bali kwa jamii na hata kwa serikali.

Kwa mara ya kwanza mwaka huu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitoa kipaumbele kuhusu maradhi hayo kwenye mjadala wake na Katibu Mkuu Ban Ki-moon amezitaka nchi zote wanachama kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha wanalinda watu wao na kuokoa maisha ya mamilioni kwa kuwa na sera bora za kudhibiti maradhi haya.

Magonjwa haya awali yalichukuliwa kuwa ni ya mataifa yaliyoendelea lakini sasa mkondo umegeuka na nchi za dunia ya tatu hasa za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara zimeanza kushuhudia ongezeko na athari za magonjwa haya.

Kisukari kwa mfano kimeenea sana Afrika ya Mashariki ikiwemo Burundi ambako takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu kumi, mmoja anasumbuliwa na kisukari.

Wananchi wanaokadiriwa laki nane wamepatwa na ugonjwa huo na isitoshe Maradhi ya kisukari yanachukua nafasi ya tatu kwa kuuwa watu wengi baada ya Malaria na Ukimwi Burundi. Na hali mbaya ya kisukari imekuwa sio mijini bali pia katika vijijini kama alivyobaini mwandishi wetu Ramadhan Kibuga.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)