Mahakama ya uhalifu wa kivita yamwanchia huru mtuhumiwa

18 Novemba 2011

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia mauwaji ya jinai yaliyofanywa nchini Cambodia hatimaye imeamuru kuwa mshatikiwa wa jinai hizo awezi kuendelea kukabiliwa na kesi hiyo kutokana na sababu za kiafya.

 Mshtakiwa huyo mwenye umri wa miaka 79 ambaye pia alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika kundi la Khmer Rouge, sasa hatasimama tena kizimbani kukabiliana na kesi yake baada ya mahakama kuridhia kuwa hali ya afya yake ni mbaya.

Mahakama hiyo ya uhalifu imetaka mshtakiwa huyo Ieng Thirith,aachiwe huru bila masharti yoyote.

Alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha mauji ya halaiki pamoja na kuziendea kinyume haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud