Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuhusu kukabilia kutokea kwa majanga yaidhinishwa:IPCC

Ripoti kuhusu kukabilia kutokea kwa majanga yaidhinishwa:IPCC

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kuzuia majanga Margareta Wahlstrom amekaribisha kuidhinishwa kwa mapendekezo ya wanachama wa IPCC kuhusu kuzuia hatari ya majanga.

Amesema kuwa kudhinishwa kwa ripoti hiyo mjini Kampala Uganda ni mwanzo mpya ya kukabilina na majanga ikiwa ndiyo ripoti ya kwanza inayotokana na kazi ya watafiti kuhusu athari za mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hii inaeleza jinsi watu walio kwenye maeneo yaliyo kwenye hatari ya kukumbwa na majanga watakavyoathirika kwenye miaka inayokuja.