IOM yataka msaada zaidi kuwahamisha wakimbizi wa Angola walioko Zambia, DRC

18 Novemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limetoa mwito likitaka kutolewa misaada zaidi ili kufanikisha jukumu la kuwarejesha wakimbizi wa Angola walioko katika nchi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Tangu mwezi June mwaka huu raia hao wa Angola wanaofikia 52,000 wameanza kurejeshwa makwao kufuatia kukamilika kwa mpango unaowataka wakimbizi hao kurejea nyumbani kwa hiari.

Kwa mujibu wa IOM, ambalo linashirikiana na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR zaidi ya dola za Marekani milioni 21 zinahitajika ili kufanikisha mchakato huo wa kuwarejesha nyumbani.

Hadi sasa IOM imepokea kiasi cha dola za kimarekani milioni 2 zinazotumika kuratibia mipango ya kuwarejesha wakimbizi hao. IOM inataka jumuiya za kimataifa kuendelea kutoa kiasi zaidi cha fedha.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter