Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migiro awataka vijana wakuhimiza viongozi wa dunia kutilia uzito maendeleo endelevu

Migiro awataka vijana wakuhimiza viongozi wa dunia kutilia uzito maendeleo endelevu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose-Migiro amewatolea mwito vijana duniani kote kutumia vyema vipaji na nguvu waliyonayo kuwatia shime viongozi wanaojiandaa kujitokeza kwenye mkutano wa mwaka ujao Umoja wa Mataifa unaotazamiwa kufanyika huko Brazil wenye shabaya kujadilia maendeleo endeleovu na utokomezaji umaskini.

Viongozi wa dunia wanakutana huko Brazil hapo mwakani kushiriki kwenze mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ambao umelenga kujadilia masuala ya maendeleo endelevu na upunguzaji umaskini.

Mkutano huo unaojulikana kama (Rio+20) unashabaa ya kuwahimiza viongozi wa duniani kuanisha sera pamoja na kuweka mikakati itayokaribisha maendeleo endelevu na kutokomeza umaskini.

Akijadilia hali hiyo, Migiro amesema kuwa vijana wananafasi kubwa ya kuwasukuma viongozi wa dunia ili watilie mkazo masuala yanayotafutiwa ufumbuzi sasa.