Rais wa zamani wa Ghana kuongoza ushirikiano na UM kuhusu mazingira na maji

17 Novemba 2011

Rais wa zamani wa Ghana John Kufuor ndiye ataongoza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa ujulikanao kama Usafi na Maji kwa wote ulio na lengo la kuhakikisha kuwa watu wanaishi kwenye mazingira safi na wanapata maji safi.

Rais Kufuor ambaye ndiye mwenyekiti wa kwanza wa ushirikiano huo anasema kuwa ndoto ya kuwahakikishia wote maji iko karibu kutimizwa lakini hata hivyo inahitaji uungwaji mkono wa kisiasa. Kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyo kwenye ushirikiano huo ni pamoja na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF , Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, shirika la mkaazi la UM UN-Habitat na chuo cha Umoja wa Mataifa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter