Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya UM yaiamrisha Ufaransa kumkamata msemaji wake wa zamani

Mahakama ya UM yaiamrisha Ufaransa kumkamata msemaji wake wa zamani

Mahama ya Umoja wa Mataifa iliyobuniwa baada ya mzozo wa Balkans wa miaka ya 90 imeiamuru Ufaransa kumkamata aliyekuwa msemaji wa mahakama hiyo ambaye alishindwa kulipa faini ya pauni 7000 aliyopewa kwa kukiuka sheria ya mahakama.

Majaji watano kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Yugoslavia ya zamani waliiamrisha Ufaransa kumtafuta na kumakata Florence Hartmann na kumsalimisha kwa mahakama hiyo iliyo na makao yake mjini Hague nchini Uholanzi. Hartmann raia wa Ufaransa alihukumiwa mwaka 2009 kwa kuchapisha kitabu na kuandika makala iliyokuwa siri kuhusu kesi cha kiongozi wa zamani wa Serbia Slobodan Milosevic.