Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wahamiaji wachangia dola bilioni 350 katika uchumi wa nchi zao:IFAD

Wafanyakazi wahamiaji wachangia dola bilioni 350 katika uchumi wa nchi zao:IFAD

Sekta za umma, binafsi na washirika wa jumuiya za kijamii wanakutana katika mkutano wa kila mwaka wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD ili kutoa changamoto kwa wahamiaji kuwekeza nyumbani walikotoka.

IFAD inasema wakati watu milioni 215 wanaishi nje ya nchi zao mapato yao yana umuhimu mkubwa katika nchi zinazoendelea, na kuyatumia vyema mapato hayo ndio ajenda kwa ya mkutano wa IFAD. Kwa mujibu wa rais wa IFAD Kanayo F. Nwanze mfuko huo unasema mpango mpya wa uwekezaji kwa waishio nje kwa ajili ya kilimo DIA unawawezesha wahamiaji kuwekeza na kujenga upya jamii zao baada ya vita na machafuko.

Ameongeza kuwa wakati wengi wanawachukulia wafanyakazi wahamiaji kama kundi lisilojiweza na lenye uwezo mdogo kifedha, lakini ukweli ni kwamba ni chachu kubwa ya mabadiliko katika nchi wanazotoka, kwani mbali ya dola bilioni 400 walizohifadhi katika benki wafanyakazi hao wahamiaji wametuma nyumbani dola bilioni 350 kusaidia familia zao katika nchi zinazoendelea mwaka huu.

Wengine wanaoshiriki mkutano huo ni taasisi za fedha, benk na makampuni yanayotuma fedha.