Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu la UM azungumzia suala la kupunguza majanga na maafisa nchini Japan

Rais wa Baraza Kuu la UM azungumzia suala la kupunguza majanga na maafisa nchini Japan

Suala la kupunguza athari za majanga ndilo limepewa kipaumbele kwenye ziara ya rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser wakati anapoendelea na ziara yake nchini Japan ambapo amekutana na maafisa wa ngazi za juu serikalini mjini Tokyo.

Kwenye mkutano kati yake na spika wa bunge la Japan Takahiro Yokomichi bwana Al-Nasser alizungumzia ujenzi mpya baada ya jango la tetemeko la ardhi na tsunami kuikumba nchi hiyo mwezi Machi. Wawili hao pia walizungumzia njia za kupunguza majanga hasa mabadiliko ya hali ya hewa suala ambalo pia lilijadiliwa kati ya Al Nasser na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Koichiro Gemba.