Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muafghanistan na Mpalestina wapata tuzo ya kuvumiliana:UNESCO

Muafghanistan na Mpalestina wapata tuzo ya kuvumiliana:UNESCO

 

Mwanamke mpigania haki kutoka Afghanistan na mwanaharakati wa masuala ya amani kutoka Palestina ndio washindi wa tuzo ya mwaka huu kwa ajili ya kuchagiza masuala ya kuvumiliana na kuepuka ghasia.

Tangazo hilo limetolewa na UNESCO katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuvumiliana inayofanyika kila mwaka Novemba 16.

Tuzo hiyo ya kuchagiza masuala ya kuvumiliana na kuepuka ghasia ni ya thamani ya dola 100,000 na itaganywa nusu kwa nusu miongoni mwa wanawake hao wawili washindi ambao ni Anarkali Honaryar kutoka Afghanistan na Khaled Abu Awwad kutoka Palestina ambaye anapigia chepuo kuvumiliana na mchakapo wa maridhiano baina ya Waisrael na Wapalestina. Siku ya kimataifa ya kuvumiliana ilianzishwa na UNESCO mwaka 1945.