Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwajumuisha katika mfumo wa elimu watoto wa wahamiaji Japan ni muhimu:IOM

Kuwajumuisha katika mfumo wa elimu watoto wa wahamiaji Japan ni muhimu:IOM

Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Laura Thomson Jumatano amehutubia kongamano mjini Tokyo Japan linalotathimini mafanikio ya mipango ya miaka mitatu ya kuwasaidia watoto wa wahamiaji kupata elimu Japan.

Mpango huo uliogharimu dola milioni 38 ni wa kusaidia kuondoa tofauti mashuleni na kujumuisha watoto hao wa wahamiaji kwenye mfumo wa elimu wa taifa hilo. Kongamano hilo limeandaliwa na IOM na wizara ya elimu, utamaduni, michezo, sayansi na teknolojia ya Japan. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)