Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi nyingi zinaongeza mipango ya kuhamia uchumi unaojali mazingira

Nchi nyingi zinaongeza mipango ya kuhamia uchumi unaojali mazingira

Wakati dunia ikijiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Rio+20, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP inaonyesha kwamba serikali nyingi na makampuni ya biashara yanaonekana yatachukua hatua ili kuchapuza mipango ya kimataifa ya kuelekea kwenye matumizi madogo ya cabon, matumizi bora ya rasilimali na kujumuisha mstakhbakali unaojali mazingira.

Ripoti inasema kuanzia Uchina hadi Barbados, Brazil hadi Afrika ya Kusini nchi zinaendeleza uchumi unaojali mazingira na shughuli ambazo zitachangia kukua kwa uchumi huo, kuleta ajira, kulinda mazingira na usawa.

Ripoti hiyo ya UNEP inayoitwa kuelekea uchumi wa kijani, njia za kuwa na maendeleo endelevu na kutokomeza umasikini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wakati macho na masikio ya dunia yakielekezwa kwenye mkutano wa Rio+20 Juni 2012, ripoti inatoa changamoto ya imani kwamba hakuna biashara baina ya uchumi na mazingira.