UM uko pamoja nanyi wakatu huu wa matatizo ya mafuriko:Thailand

16 Novemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliye ziarani nchini Thailand amewahakikishia wananchi na serikali ya Thailand kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili kutokana na mafuriko.

Amesema amesikitishwa sana na hali halisi aliyoishudia na kwamba kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi kwa karibu na kitengo cha majanga cha nchi hiyo kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kwa msaada wowote utakaohitajika ili kunusuru maisha ya watu zaidi na kuwasaidia kurejea katika hali ya kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa pamoja na waziri mkuu wa Thailand Ban ametoa salamu za rambirambi kwa jamaa wa waliopoteza maisha na kuwatia moyo waliopoteza kila kitu katika mafuriko hayo. Pia ameishukuru jumuiya ya kimataifa kwa msaada wao.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter