Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa kukomesha mabomu mtawanyiko unaonekana kufanya kazi

Mkataba wa kukomesha mabomu mtawanyiko unaonekana kufanya kazi

Mkataba wa kimataifa unaopiga marufuku matumizi ya mabomu mtawanyiko umeanza kuzaa matunda mwaka mmoja tu baada ya kuanza kutekelezwa rasmi kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya mwaka 2011 inayofuatilia mabomu hayo ambayo imezinduliwa Jumatano mjini Geneva.

Ripoti inaonyesha jinsi gani serikali zilizojiunga na mkataba huo zinavyoutekeleza kwa makini na hamasa kubwa amesema Steve Goose mwenyekiti wa muungano wa kukabiliana na mabomu mtawanyiko na pia mhariri wa ripoti hiyo.

Amesema hatua zimepigwa kuanzia katika kuharibu maghala ya mabomu hayo hadi kuweka sheria za kuyapinga. Amesema wanashuhudia mataifa yakikumbatia mkataba huo kwani hadi sasa mataifa 111 yameshajiunga yakikubali kupiga marufuku silaha hizo.

(SAUTI YA STEVE GOOSE)

Ripoti hiyo imezinduliwa katika mkutano uliowaleta pamoja wanadiplomasia kutoka nchi zaidi ya 100 mjini Geneva wiki hii wakijadili mipango ya kuhakikisha mabomu mtawanyiko yanatokomezwa kabisa. Marekani na baadhi ya nchi wanatia shinikizo kuwe na mkataba mpya utakaoruhusu kuelendelea kutumia, kuzalisha na biashara ya mabomu hayo lakini nchi nyingi duniani zinapinga.