Familia za wakimbizi wa ndani Jamhuri ya Afrika ya kati zakumbwa na ugumu wa maisha

Familia za wakimbizi wa ndani Jamhuri ya Afrika ya kati zakumbwa na ugumu wa maisha

Baraza moja linalohusika na wakimbizi kutoka nchini Denmark limesema kuwa hali kimaisha ya wakimbizi karibu na mji wa Ndele ulio Kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati ni ngumu likisema kuwa kuna visa vingi vya kuolewa kwa watoto na ajira za watoto.

Kulingana na uchunguzi wa shirika hilo uliofanyiwa watu 17,000 uligundua kuwa moja kati ya familia tano zimempoteza mmoja wao mwaka huu kutokana na ukosefu wa usalama na huduma za afya na pia kutokana na ukosefu wa chakula.

Familia hizo zinasema kuwa ziliwaoza watoto wao wa kike kwa wenyeji wa eneo hilo na kuwatuma watoto kufanya kazi kwa mashamba yao ili wapate chakula na pesa. UNHCR inasema kuwa kumeripotiwa visa vya ubakaji unaondeshwa na makundi yalijihami. Msemaji wa UNHCR anasema shirika hilo linamatumaini kwamba kuimarika kwa usalama kutaruhusu huduma kutolewa kwa wakimbizi.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)