Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu waripotiwa kwenye kambi ya Daadab

Ugonjwa wa kipindupindu waripotiwa kwenye kambi ya Daadab

Mtu mmoja ameripotiwa kuaga dunia kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya kufuatia kutokea mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema mvua kubwa inayonyesha eneo hilo inaendelea kutatiza juhudi za utoaji wa huduma kwenye kambi hii.

Msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic anasema kuwa makundi ya kutoa misaada yanaendelea na juhudi za kurejesha huduma hata baada ya kutokuwepo usalama wa kutosha nje na ndani mwa kambi.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)