Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan na Sudan Kusini wanahitaji mipango madhubuti ya kuishi pamoja

Sudan na Sudan Kusini wanahitaji mipango madhubuti ya kuishi pamoja

Mkuu wa huduma za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema kuwa mataifa ya Sudan na Sudan Kusini ni lazima yawe na mikakati ya kuishi pamoja kwa amani. Kumekuwa na hali ya wasiwasi hivi majuzi kati ya nchi hizo mbili kufuatia mashambulizi ya angani yaliyofanywa na vikosi vya Sudan wiki iliyopita kwenye kambi ya wakimbizi nchini Sudan Kusini.

Bwana Ladsous aliiambia radio ya Umoja wa Mataifa kwamba uhusiano kati ya mataifa hayo ni lazima upewe kipaumbele baaada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake kutoka Sudan mwezi Julai mwaka huu.