Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za binadamu zinaathiri maisha ya wanyama wanaohamahama:UNEP

Shughuli za binadamu zinaathiri maisha ya wanyama wanaohamahama:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingiza UNEP linasema shughuli zinazofanywa na binadamu zinaendelea kuathiri maisha ya wanayama wanaohamahama duniani.

Shirika hilo linasema masula ya ujenzi wa barabara, uvuvi, uwekaji wa nguzo za umeme, uchimbaji visima na uchaguzi wa mazingiza ni baadhi ya vikwazo kwa wanayama hao kama ndovu, ndege na viumbe wengine wa majini na nchi kavu.

Kila mwaka kwa mujibu wa UNEP aina 10,000 za viumbe wakiwemo wanyama na ndege huama kutoka nchi moja kwenda nyingine na wengine kutoka bara moja kwenda lingine.

Afisa habari na mawasiliano wa UNEP Nairobi Waiganjo Njoroge anasema wameanzisha mradi maalumu kuwalinda viumbe na wanyama hao wanaohama.

(MAHOJIANO NA WAIGANJO NJOROGE)