Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangladesh imepiga hatua kubwa katika miongo minne:Ban

Bangladesh imepiga hatua kubwa katika miongo minne:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarani nchini Bangladesh amesema taifa hilo la Asia limepiga hatua kubwa katika kipindi cha miongo mine. Amesema na mabadiliko yanaonekana katika kuelekea utulivu wa kisiasa na ukuaji wa uchumi. Ban ameliambia taifa hilo kuwa hatua walizopiga kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ni za kujivunia na mfano wa kuigwa na mataifa mengine, na pia Bangladesh inaongoza kwa maandalizi ya kukabiliana na mjanga duniani.

Akitoa mfano amesema mwaka 1991 kimbunga kilichokumba Bangladesh kilikatili maisha ya watu 140,000 lakini kimbunga Sidrk cha mwaka 2007 kilidhibitiwa na watu wengi kuokolewa 4000 pekee ndio waliopoteza maisha. Kwa sababu ya maandalizi mazuri mamilioni ya watu wa Bangladesh wako salama zaidi wakati huu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)