Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ataka uchunguzi ufanyike dhidi ya shambulio la bomu kambini Sudan Kusini

Pillay ataka uchunguzi ufanyike dhidi ya shambulio la bomu kambini Sudan Kusini

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo Ijumaa ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa shambulio la mabomu la anga lililotokea Alhamisi kwenye kambi ya wakimbizi jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.

Pillay amesema taarifa walizonazo hadi sasa zinaashirika kwamba shambulio hilo huenda likwa ni uhalifu wa kimataifa au ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu. Katika kambi hiyo kulikwepo na maelfu ya raia wakiwemo wanawake na watoto, na idadi kamili ya waliokufa au kujeruhiwa haijajulikana ingawa imefahamika kwamba mabomu matano au sita yalidondoshwa kambini hapo na moja lilianguka karibu na shule.

Pillay ameelezea hofu dhidi ya mashambulizi ya kibaguzi na mapigano ambayo yanaendelea kwenye mpaka katika jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan na kusambaa kwenye majimbo ya jirani. Amezitaka pande zote husika kwenye mapigano kusitisha mara moja mashambulizi dhidi ya raia.