Kundi la UM kusherehekea miaka 20 ya kutetea wafungwa

11 Novemba 2011

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza kuzuiliwa kwa watu bila sababu litasherehekea miaka 20 ya mafanikio yake mnano tarehe 14 mwezi huu na kuangazia changamoto zilizo mbeleni kwenye sherehe zitakazoandaliwa mjini Paris.

Kati ya vizuizi vilivyofanyiwa uchunguzi ni pamoja na kuzuiliwa kwa Aung San Suu Kyi, Xanana Gusmao miongoni mwa wengine ambapo baadhi yao waliachiliwa. Wawili kati ya wale kesi zao zilichunguzwa na kundi hilo watahudhuria sherehe hiyo wakiwemo Haithaman al- Maleh kutoka Syria na Birtukam Mideksa kutoka Ethiopia huku Aung San Suu Kyi akitarajiwa kuwasilisha ujumbe wake kwa njia ya Video.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter