Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zapigwa kwenye vita dhidi ya Pneumonia

Hatua zapigwa kwenye vita dhidi ya Pneumonia

Siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Pneumonia ikisherehekewa hapo kesho utafiti mpya ulitolewa hiyo jana unaonyesha kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye nchi zinazoendelea itaokoa maisha ya mamilioni ya watu.

Kulingana taarifa iliyochapishwa kwenye makala ya International Health ni kwamba chanjo hizo zinazotolewa kwa nchini maskini zaidi duniani kutokana na usaidizi wa shirika la GAVI zitaokoa maisha ya kati ya watoto milioni 3 hadi 4 kwa muda wa miaka kumi ijayo.

Ripoti tofauti kutoka kwa kituo cha kimataifa la chanjo kwenye chuo cha Johns Hopkins inaonyesha kuwa hakujakuwa na usawa katika utoaji wa chanjo huku kukiwa na ukosefu wa madawa kwenye maeneo ambayo watoto wako kwenye hatari ya kuugua Pneumonia. Jeffrey Rowland ni mkurugenzi wa habari na mawasiliano kwenye shirika la GAVI.

(SAUTI YA GAVI JEFFREY ROWLAND)