Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza yafadhili IOM katika utoaji wa misaada Pakistan

Uingereza yafadhili IOM katika utoaji wa misaada Pakistan

Idara ya maendeleo ya kimataifa kutoka Uingereza DFID imelipa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM dola milioni 6.4 zitakazosaidia katika utoaji wa misaada ya dharura ya makao kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko kwenye mkoa wa Sindh nchini Pakistan.

Fedha hizo pia ziatatumiwa kuwanunulia waathiriwa bidhaa za nyumbani na mablanketi. Idara hiyo ya DFID pia inatoa ufadhili wa bidhaa za kujenga makaazi ya familia zingine 37,440 na makao mengine 7,800 kwenye wilaya za Sindh ambayo yatakuwa makao ya watu 54,600.