Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalaani mashambulizi kwenye kambi nchini Sudan

UNHCR yalaani mashambulizi kwenye kambi nchini Sudan

 

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limelaani shambulizi la anga lililofanywa kwenye kambi ya wakimbizi kwenye jimbo la Unity, Sudan Kusini. Hii ni baada ya mabomu kadhaa kudondoshwa na ndege kwenye kambi ya muda iliyo makao ya zaidi ya wakimbizi 20,000 waliokimbia ghasia kwenye milima ya Nuba iliyo kwenye jimbo la Kordofan.

Kwa sasa UNHCR imekuwa kwenye harakati za kuwatafutia wakimbizi maeneo mapya tangu kufanywa kwa shambulizi hilo hiyo jana. UNHCR inasikitishwa na kuendelea kuongezeka kwa ghasia kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini ambapo maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)