Ofisi ya haki za binadamu inasikitishwa na kutokuwepo na uhuru wa kuongea nchini Misri

11 Novemba 2011

 

Baada ya kufutialia kwa karibu hali nchini Misri tangu kuondolewa madarakani kwa rais Hosni Mubarak Ofisi ya haki binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa hakujakuwa na haki ya kusema nchini humo. Ofisi hiyo inasema kuwa mfano ni pale mwanaharati Alaa Abdel – Fatah alipokamatwa , akahukumiwa na kufungwa baada ya kulishutumu jeshi kulingana na jinsi lilivyokabiliana na waandamanaji mwezi uliopita.

Ofisi hiyo sasa inasema kuwa utawala wa mpito nchini Misri ni lazima uheshimu haki ya kusema na kujieleza kama moja ya njia za kuhakikisha kuwa uchaguzi unaokuja utakuwa wa haki. Rubert Colville ni msemaji wa ofisi hiyo.

(SAUTI YA RUPERT COLLIVE)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter