Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubunifu unahitajika zaidi kuweza kuokoa mazingira:UNEP

Ubunifu unahitajika zaidi kuweza kuokoa mazingira:UNEP

Wakati ulimwengu unapokabiliwa na changamoto za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa mashirika ya kimataifa na nchi wanaendelea kutafuta mbinu za kukabiliana na hali hiyo.

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limekuwa kwenye mstari wa mbele katika kuhamasisha na kutafuta njia ambazo zinaweza kuchangia kuzuia uharibifu wa mazingira.

Makala ya wiki hii inaangazia mradi wa mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya wa jiko la kupikia lisilotumia kuni wa makaa ambao ni moja ya miradi iliyofanikiwa kupata tuzo katika maonyesho yaliyoandaliwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye mji wa Leverkusen nchini Ujerumani ambapo miradi minne bora ilitunukiwa. Ungana naye Jason Nyakundi ili kufahamu zaidi kuhusu mradi huu.