Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apeleka timu kutathmini tishio la uharamia ghuba ya Guinea

Ban apeleka timu kutathmini tishio la uharamia ghuba ya Guinea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepeleka timu kutathimini ukubwa wa tishio la uharamia kwenye ghuba ya Guinea na kutoa mapendekezo ya uwezekano wa msaada wa Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo hilo.

Timu hiyo ya tathimini imepelekwa Guinea kufuatia ombi la Rais Boni Yayi wa Benin. Na timu hiyo inaongozwa na mkurugenzi wa kitengo cha Afrika kwenye idara ya siasa ya Umoja wa Mataifa Sammy Kum Buo na Mariam Sissoko mwakilishi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na madawa UNODC nchini Nigeria.

Timu hiyo itazuru Cotonou Benin, Abuja Nigeria, Libreville Gabon na Luanda Angola ambako watakutana na wawakilishi wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS na ile ya nchi za Afrika ya Kati ECCAS.