Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM inatoa muongozo kwa mataifa kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi ya kemikali

Ripoti ya UM inatoa muongozo kwa mataifa kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi ya kemikali

Msaada wa kiufundi unaotolewa kwa nchi kupambana na mashambulio ya kigaidi ya silaha za kemikali au kibaolojia lazima uratibiwe ipasavyo imesema ripoti mpya iliyotolewa Alhamisi na Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo inayoangalia jinsi mataifa yanavyokabiliana na ugaidi wa kutumia silaha za kibaolojia au kemikali imebainisha njia za kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na mataifa pamoja na njia mbalimbali za kuzuia mashambulizi kama hayo.

Ripoti pia inasema kwamba juhudi zaidi zinapaswa kuongezwa katika ujenzi mpya baadha ya mashambulizi hususani ikizingatiwa kwamba maeneo mengi ya mijini yatakuwa yameathirika na kemikali hizo.