UNESCO kutumia simu za mkononi kuchagiza elimu kwa wote

UNESCO kutumia simu za mkononi kuchagiza elimu kwa wote

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Nokia na Pearson Foundation wamezindua suala la elimu ya msingi kuwa ndilo wanalolipa kipaumbele katika changamoto ya elimu kwa wote yaani EFA.

Leo Novemba 10 EFA imependekeza jinsi gani mawasiliano ya simu za mkononi yanaweza kusaidia kufikia lengo la elimu ya msingi kwa wote. Mawazo kadhaa yameshatolewa katika awamu ya kwanza ya mradi huo ambao una lengo la kutafuta njia za kutumia simu za mkononi kufuta ujinga.

Katika awamu ya pili ya mradi huo wataalamu wa elimu, waalichu, wazazi, wanafunzi na waundaji wa software wamealikwa kushiriki kwa kutoa mapendekezo ya kutumia simu za mkononi kuimarisha elimu ya msingi kwa wote pia kupiga kura au kutoa maoni yao kuhusu mawazo yatakayopendekezwa.