Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matetemeko mawili mengine yakumba mji wa Uturuki:OCHA

Matetemeko mawili mengine yakumba mji wa Uturuki:OCHA

Matetemeko ya ardhi mawili yameukumba mji wa Van usiku wa kuamkia leo nchini Uturuki yakiwa na ukubwa wa vipimo vya rishta 5.6 na 4.5. Majengo 25 yameporomoka zikiwemo hoteli mbili za Bayram na Aslan na kwa mujibu wa duru za habari bado kuna watu wamenaswa kwenye kifusi na juhudi za kuwatafuta na uokozi zinaendelea.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA mitetemo mingine 1400 iletikisa eneo hilo tangu kutokea kwa tetemeko kubwa Oktoba 23 lililouwa watu zaidi ya 600 na kuwaacha maelfu bila makazi.

Maafisa wa msalaba mwekundu nchini Uturuki wanasema watu 25 wameokolewa na saba wamekufa, lakini bado haijafahamika ni watu wangapi hasa wamenaswa kwenye kifusi. Elizabeth Brys ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)