Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande husika katika vita vya Somalia zatakiwa kuzingatia athari kwa raia:UNHCR

Pande husika katika vita vya Somalia zatakiwa kuzingatia athari kwa raia:UNHCR

Pande zinazohusika katika vita vya Somalia zinaweza kuchukua hatua za haraka kupunguza athari za vita hivyo kwa raia limesema shirika la CIVIC lenye makao yake Wanshington Marekani katika ripoti yake iliyotolewa Alhamisi iitwayo athari kwa raia nchini Somalia.

Shirika hilo linaelimisha kwa niaba ya raia waliokumbwa na vita. Ripoti hiyo inabainisha njia muafaka za kuchukuliwa dhidi ya mahitaji ya Wasomali walioathirika na vita. Utafiti wa ripoti hiyo umefanywa kwa msaada wa kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na matokeo yake yametokana na kuwahoji watu 100 wakielezea hali inayowakabili kwa kuishi Somalia na hamu ya kuwa na mfumo wa kawaida utakaoshughlikia mahitaji ya waathirika.

Ripoti inasema hakuna kitakachoweza kujeresha waliyopoteza raia wa Somalia kutokana na vita.