Baraza la Usalama latakiwa kuongeza juhudi za kuleta mabadiliko ya masuala ya kisiasa

10 Novemba 2011

Wito umetolewa wa kuhakikisha vikwazo vya kuleta mabadiliko katika Baraza la Usalama vinamalizika. Wito huo umetolewa na wajumbe wa Baraza Kuuu la Umoja wa Mataifa waliokutana Jumatano jioni kuhitimisha mjadala wao wa kila mwaka kuhusu ajenda ya mabadiliko.

Wajumbe wa Baraza Kuu wanataka Baraza la Usalama ambalo halifajanyiwa mabadiliko kwa nusu karne kwenda sambamba na hali halisi ya siasa za sasa na changamoto zinazoukabili Umoja wa Mataifa katika karne ya 21. Wametaka hatua za haraka za muafaka wa mabadiliko zifikiwe ili waweze kushughulikia matatizo yaliyopo duniani kwa umakini zaidi. Nchi za Afrika ambazo ni zaidi ya nusu ya wanachama wa Umoja wa Mataifa na ambazo ndio ajenda inayotawala Baraza la Usalama hadi sasa haina mjumbe wa kudumu kati ya wajumbe 15 wa Baraza la Usalama. Mwakilishi wa Nigeria kwenye Umoja wa Mataifa alikuwa na haya.

(MWAKILISHI WA NIGERIA)

Mjadala wa kutaka mabadiliko kwenye Baraza la Usalama umekuwa ukiendelea kwa miongo miwili sasa. Wajumbe wanataka kuwe na uwiano wa uwakilishi na kusiwe na nchi inayon’gan’gania ugavi wa madaraka.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter