Rais wa Baraza Kuu ataka nchi ziendelee kupigania mageuzi ndani ya UM

9 Novemba 2011

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ametaka nchi wanachama wa Umoja huo kuendelea kutilia mkazo majadaliano ya wazi kwa shabaya ya kulijenga upya baraza la usalama litakalochukua sura ya uwajibikaji, uwazi, uwakilishi sawa na utendaji kazi wa kidemokrasia.

Bwana Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema wakati ambapo majadiliano ya kupanua idadi ya wawakilishi kwenye chombo hicho yakianza kupata msukumo mpya, kuna haja kwa nchi wanachama kuendelea kuzunguzia suala hilo tena katika hali ya uwazi na kuzingatia majadiliano.

Kumekuwa na majadiliano ya hapa na pale pamoja na miito toka sehemu mbalimbali duniani inayotaka kufanyika mageuzi ndani ya chombo hicho ambacho hakina uwakilishi unaowiana wa wanachama.

Rais huyo amesisitiza umuhimu wa kuyakubali mageuzi hayo akisema kuwa muundo wa sasa wa chombo hicho haujafaulu kutatua changamoto zinazoendelea kuikabili dunia kwa wakati huu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter