Wote wana haki ya kuwa na maendeleo duniani:Pillay

9 Novemba 2011

Maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wamesisitiza umuhimu wa kufanya mamendelo kuwa kitu cha kuaminika kwa kila mmoja , popote pale ili kuhakikisha kuwa yameleta mabadiliko kwa maisha ya mabilioni kote duniani.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa wakati karibu watu bilioni tatu wanaendelea kuishi kwenye umaskini asilimia 20 ya watu ndio wanamiliki asilimia 70 ya pato la dunia ishara kuwa ahadi hazijatimizwa. Ameongeza kuwa huu ndio wakati wa kuwekeza kwenye maendelo na kwa watu hususan wanawake na vijana kwa kuwa wanachukua asilimia kubwa ya watu walioko duniani.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud