Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 50 ya samaki wanaoliwa duniani wanatokana na kilimo cha viumbe vya majini:FAO

Asilimia 50 ya samaki wanaoliwa duniani wanatokana na kilimo cha viumbe vya majini:FAO

Ripoti ya mwaka 2010 ya shirika la kilimo na chakula FAO kuhusu kilimo au ufugaji wa viumbe vya majini duniani inasema ifikapo mwaka 2012 zaidi ya asilimia 50 ya samaki wote wanaoliwa duniani itatokana na kilimo au ufugaji wa samaki.

Ripoti inasema kutokana na kuzorota kwa sekta ya uvuvi na ongezeko la uharibifu wa hali ya hewa ufugaji wa samaki unaonekana utakuwa na umuhimu mkubwa wa kuzalisha samaki katika siku za usoni ili kukidhi mahitaji na usalama wa chakula cha viumbe vya majini.

Kwa mujibu wa FAO ufugaji wa samaki unazalisha karibu nusu ya samaki wote wanaoliwa duniani. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)