Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast leo ameziomba pande zote husika nchini humo kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao unakuwa wazi, huru na kujumuisha wote.
Bert Koenders amesema leo hii taifa hilo la Afrika ya Magharibi lina Rais aliyechaguliwa na kinachohitajika sasa ni bunge lililochaguliwa na linalojumuisha mitazamo tofauti ya kisiasa.
Bwana Koenders ambaye pia ni mkuu wa operesheni za Umoja wa mataifa nchini humo UNOCI ametoa kauli hiyo kufuatia mkutano wake na Rais Alassane Ouattara mjini Abidjan.
Uchaguzi huo utakaofanyika December 11 ulikuwa ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika mkutano wao. Pia wamejikita katika masuala ya ufufuaji wa uchumi na usalama katika taifa hilo.