Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa ya maziwa makuu yaafikiana mbinu za kukabili makundi ya waasi

Mataifa ya maziwa makuu yaafikiana mbinu za kukabili makundi ya waasi

Mataifa 11 yanayojumuika kwenye kongamano la kimataifa la maziwa makuu yameazimia uundwaji wa kituo cha pamoja cha ujajusi katika eneo hilo .

Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikichagizwa na Umoja wa Mataifa kupata sulhu ya makundi ya waasi kama FDLR, LRA wa ganda na mengineyo yanayotishia usalama itakuwa na makao yake maku mjini Goma –DRC na dhamira yake itakua ni kukusanya na kupeana habari kwa mataifa hayo kuhusu harakati za vikundi haramu vya eneo hilo.

Vilevile Mataifa hayo yameafikiana kufuatilia karibu hali nchini Somalia ambayo wameitaja kama kitisho kikubwa cha utengamano katika maziwa makuu baada ya nchi kadhaa za jumuiya hiyo kuingilia kati katika mzozo huo.

Ili kutaka kujua mengi kuhusu maazimio ya mkutano huo uliofanyika mjini Bujumbura,muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA amezungumza na Stephen SINGO,msimamizi wa kitengo cha amani na usalama katika kongamano la kimataifa la Maziwa Makuu ICGLR.

(MAHOJIANO NA STEPHEN SINGO)