Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lashangazwa na kushindwa kuondolewa kwa vikosi kutoka Abyei

Baraza la Usalama la UM lashangazwa na kushindwa kuondolewa kwa vikosi kutoka Abyei

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea masikitiko yake na kushindwa kwa serikali za Sudan na Sudan kusini katika kuondoa vikosi vyao kutoka eneo lilalozozananiwa la Abyei ambapo limezitaka nchi hizo kufanya hima kuondoa vikosi vyao bila masharti. Hata hivyo Baraza hilo la Umoja wa Mataifa limekaribisha kupelekwa kwa kikosi cha kulinda amani cha UM cha UNISFA kwenye eneo la Abyei na usaidizi unaotolewa na Serikali ya Ethiopia.

Nayo UNISFA imetakiwa kuongeza doria pamoja na shughuli zake za angani. UM pia unazitaka nchi hizo mbili kushirikiana katika kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Abyei.