Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira huharibika zaidi wakati wa mizozo:Ban

Mazingira huharibika zaidi wakati wa mizozo:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa mazingira ndiyo hupata pigo kubwa hususani wakati wa vita.  Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuzuia uharibifu wa mazingira wakati wa mizozo Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa umepiga hatua kubwa katika kuleta ufahamu kuhusu uhusiano uliopo kati ya vita na mazingira na mchango wa mali asili kwenye uchochezi wa mizozo.

Ban anaonya kuwa mataifa yenye misukosuko hasa yaliyokumbwa na mapigano huenda yakakabiliwa na uhaba wa mali asili miongo inayokuja akiongeza kuwa mahitaji ya mali asili yanaendelea kuongezeka hali inayosabishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu duniani.