Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha kusafirisha misaada kwenda Somalia chafunguliwa Dubai

Kituo cha kusafirisha misaada kwenda Somalia chafunguliwa Dubai

Kituo kipya kitakachotumiwa kusafirisha misaada ya kibinadamu kwenda nchini Somalia kimefunguliwa mjini Dubai. Inakadiriwa kuwa takriban tani 5000 za unga zitapitia kwenye kituo hicho kila mwezi kuwalisha watoto mwenye sehemu zilizoathirika zaidi na ukame kwenye taifa hilo la pembe ya Afrika. Kituo hicho kimefunguliwa na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

UNICEF inasema kuwa inakabiliwa na changamoto za usafiri katika kuwapelekea chakula watoto walio kwenye hatari ya kufa njaa nchini Somalia. Shirika hilo linasema kuwa kwa sasa kuna takiban watoto milioni 1.5 Kusini mwa Somalia wanaohitaji msaada wa chakula.