Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha wahamiaji kutoka mjini Tripoli

IOM yasafirisha wahamiaji kutoka mjini Tripoli

Kundi la wahamiaji 332 waliokuwa wamekwama kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli kufuatia mzozo ulioshuhudiwa nchini humo wamesafirishwa kwa njia ya ndege kutoka nchini humo na ndege mbili za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Wote hao waliwasili kwenye mji wa Niamey nchini Niger na ndilo kundi la kwanza la wahamiaji kusafirishwa miongoni mwa takriban wahamiaji 2000 raia wa Niger ambao ubalozi wa Niger unaamini wamesalia mjini Tripoli. IOM imeshirikiana na utawala nchini Libya pamoja na maafisa wa ubalozi kuwafikia wahamiaji hao kabla ya kupewa vyeti vya usafiri. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)